Punguza makosa, wekeza kwa wakati halisi, toa huduma bora kwa wanachama wako kwa mfumo wa SIMAS
Mfumo kamili wa usimamizi wa SACCOS unaojumuisha kila kitu unachohitaji
Hifadhi taarifa za wanachama, hisa, na akiba kwa urahisi. Fanya usajili, uhakiki na uboreshaji wa data ya wanachama.
Dhibiti mchakato wote wa mikopo kuanzia maombi, uhakiki, idhini, hadi malipo ya marejesho na ripoti.
Angalia mapato na matumizi, tengeneza bajeti, fanya uchambuzi wa kifedha na upate ripoti za kiotomatiki.
Tuma arifa, matangazo na ukumbusho kwa wanachama wako kupitia SMS moja kwa moja kutoka kwenye mfumo.
Wanachama na wasimamizi wanaweza kufikia mfumo kupitia simu za mkononi kwa urahisi na usalama.
Pata miongozo ya haraka na sahihi ya hali ya SACCOS yako wakati wowote na popote.
SIMAS ni mfumo wa kimtandao uliobuniwa kwa ajili ya kuendesha, kudhibiti, na kuhifadhi taarifa pamoja na miamala ya SACCOS.
Mfumo huu umejengwa kwa teknolojia ya kisasa na kusudi la kuwawezesha wakuu wa SACCOS kufanya kazi kwa urahisi, usahihi na uwazi zaidi.
Tunatoa mfumo madhubuti unaozingatia uwazi, usahihi wa taarifa, utoaji wa huduma bora kwa mtumiaji, na utoaji wa taarifa kwa wakati halisi (papo kwa papo).
Uboreshaji wa utendaji kazi wa SACCOS
Upunguzaji wa makosa ya kibenki
Urahisishaji wa mchakato wote wa usimamizi
Zaidi ya SACCOS 100 nchini Tanzania zimetumia mfumo wa SIMAS
Maoni kutoka kwa SACCOS zinazotumia SIMAS
"Tumekuwa tukitumia SIMAS kwa miaka sita sasa na imetupa ufanisi mkubwa katika usimamizi wa wanachama na mikopo. Mfumo huu ni rahisi kutumia na una uwezo wa kutosha."
"Kwa kutumia SIMAS, tumepunguza muda wa kufanya kazi kwa zaidi ya 50%. Sasa tunaweza kufocus zaidi kwa kuhudumia wanachama badala ya kufanya kazi za kutumia makaratasi kwa muda mrefu."
"Bulk SMS ya SIMAS imetuwezesha kuwa karibu na wanachama wetu kwa urahisi. Sasa tunaweza kuwatuma taarifa muhimu kwa wakati na kupunguza gharama za uenezi."
Jinsi mfumo wetu unavyokidhi mahitaji ya SACCOS kwa ufanisi
SIMAS inatumia mbinu za kimataifa za usimamizi wa mikopo na akiba zilizoidhinishwa na taasisi za kifedha.
Uboreshaji wa kila siku kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu kama AI(Artificial Intelligence).
Mazoezi ya kuwajengea uwezo wa watumiaji kwa kutumia mbinu mpya za kidijitali.
Tuna demo ya bure ambayo inakuwezesha kujionea jinsi mfumo unavyofanya kazi kabla ya kufanya maamuzi.
Jisikie huru kujaza fomu hapa chini na tutakutumia maelekezo ya kuingia kwenye mfumo wa demo.
Demo ya bure bila malipo
Maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa mtaalamu wetu
Hakuna mikataba ya lazima
Tunakaribisha maswali yako na maoni kuhusu SIMAS
Cohema Company Limited, Iringa, Tanzania
+255 761 610 188
info@cohema.co.tz
Jumatatu - Ijumaa: 8:00 asubuhi - 5:00 jioni